Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Bani Israil 17:71

17:71
يوم ندعو كل اناس بامامهم فمن اوتي كتابه بيمينه فاولايك يقرءون كتابهم ولا يظلمون فتيلا ٧١
يَوْمَ نَدْعُوا۟ كُلَّ أُنَاسٍۭ بِإِمَـٰمِهِمْ ۖ فَمَنْ أُوتِىَ كِتَـٰبَهُۥ بِيَمِينِهِۦ فَأُو۟لَـٰٓئِكَ يَقْرَءُونَ كِتَـٰبَهُمْ وَلَا يُظْلَمُونَ فَتِيلًۭا ٧١
يَوۡمَ
نَدۡعُواْ
كُلَّ
أُنَاسِۭ
بِإِمَٰمِهِمۡۖ
فَمَنۡ
أُوتِيَ
كِتَٰبَهُۥ
بِيَمِينِهِۦ
فَأُوْلَٰٓئِكَ
يَقۡرَءُونَ
كِتَٰبَهُمۡ
وَلَا
يُظۡلَمُونَ
فَتِيلٗا
٧١
Siku tutapo waita kila kikundi cha watu kwa mujibu wa wakifuatacho - basi atakaye pewa kitabu chake kwa mkono wake wa kulia, basi hao watasoma kitabu chao wala hawatadhulumiwa hata chembe. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na kumbuka, ewe Mtume, Siku ya Kufufuliwa, kwa njia ya kutoa bishara na kuogopesha, pindi Mwenyezi Mungu, Aliyeshinda na ktukuka, Atakapoliita kila kundi la watu pamoja na kiongozi wao ambaye walikuwa wakimfuata ulimwenguni. Basi aliyekuwa mwema kati yao , na akapewa kitabu chake kwa mkono wake wa kulia, hawa watasoma kitabu cha mema yao wakiwa katika hali ya kufurahika na kuterema, na kamwe hawatapunguziwa chochote katika malipo ya matendo yao mazuri, hata kama ni kadiri ya uzi unaokuwa kwenye mpasuko wa koko ya tende.